Home
Home
Podcasts
Podcasts
Library
Cancel
Sign in
Elimu
The Standard Group PLC
Follow
Inahusu masuala yote elimu; sera, mtalaa, ubunifu, vipaji, utafiti, uandishi, mitihani, ajira, vyama na taasisi za elimu, changamoto na suluhu.
read less
Start Here
Aug 27 2022
CBC irekebishwe; Humphrey Obarah
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Talanta Duniani Profesa Humphrey Oborah, ambaye alivumbua kifaa cha kupima talanta na uwezo wa mwanafunzi kimasomo anaiataka serikali mpya kuifanyia sekta ya elimu nchini mageuzi ili kuhakikisha kuwa inaafikia malengo yake. Obarah anapendekeza Wizara ya Elimu kufanyiwa marekebisho na kuundwa kwa Wizara ya Masomo ambayo itahakikisha kuwa mageuzi yanafanyika katika sekta ya elimu nchini. Kwenye mazungumzo na Faith Kutere, Oborah aidha anapendekeza Mtaala wa Umilisi CBC kurekebishwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora.
Aug 27 2022
CBC irekebishwe; Humphrey Obarah
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Talanta Duniani Profesa Humphrey Oborah, ambaye alivumbua kifaa cha kupima talanta na uwezo wa mwanafunzi kimasomo anaiataka serikali mpya kuifanyia sekta ya elimu nchini mageuzi ili kuhakikisha kuwa inaafikia malengo yake. Obarah anapendekeza Wizara ya Elimu kufanyiwa marekebisho na kuundwa kwa Wizara ya Masomo ambayo itahakikisha kuwa mageuzi yanafanyika katika sekta ya elimu nchini. Kwenye mazungumzo na Faith Kutere, Oborah aidha anapendekeza Mtaala wa Umilisi CBC kurekebishwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora.
Apr 28 2022
Wanafunzi pacha; alama sawa, KCPE na KCSE
Brooke na Chelsea Sagala ni pacha ambao wamekuwa wakipata alama sawa au zinazokaribiana tangu walipoanza masomo. Wawili hawa walipata gredi ya B- ya alama 57 na kupata alama sawa kwenye masomo yote katika KCPE. Aidha, walipata alama sawa ya 380 kwenye mtihani wa KCPE. Faith Kutere amezungumza na pacha hawa ambao wanasema kuwa licha ya kutia bidii na kushindana masomoni, wamekuwa wakipata alama sawa. Wawili hawa wanalenga kujiunga na Chuo Kikuu cha Katoliki na kusomea uanasheria wakiwa na matumaini kuwa hawatatenganishwa na chochote maishani.
Mar 3 2022
Elimu ya kiufundi Ukraine; fursa za ajira ni chache - Paul Kurgat
Paul Kurgat aliwahi kuwa Balozi wa Kenya nchini Ukraine na pia alisomea Ulaya, hasa Urusi. Kwenye Elimu Podcast, Balozi Kurgat anazungumza na Faith Kutere kuhusu elimu nchini humo na kulinganisha na mfumo wa elimu nchini Kenya. Pia anaeleza jinsi ambavyo vita kati ya Ukraine na Urusi vitakavyowaathiri wanafunzi wanaosomea huko.
Jan 20 2022
Elimu: Siku ya Kiswahili Duniani (UNESCO); tukitumie ofisini, siasani....
Kiswahili ambacho ni lugha ya kitaifa na rasmi nchini Kenya kinazidi kupiga hatua duniani licha ya changamoto mbalimbali kuhusu matumizi yake nchini Kenya. Hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya lugha hii ni kuhusu Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuipa hadhi lugha hii kwa kutangaza Julai saba kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani. Mwaka wa 2021, magwiji na wakereketwa mbalimbali wa Kiswahili nchini Kenya wamezidisha sauti zao kuhusu haja ya Kiswahili kutumiwa katika mazingira rasmi kwani ni dhahiri kuwa Kiingereza kingali kupaumbele cha wengi katika maeneo ya kazi. Geoffrey Mung’ou ameandaa makala maalumu kuhusu hali ya Kiswahili, hatua zilizopigwa na yanayohitajika kufanywa ili kukabili changamoto kukihusu.
Nov 13 2021
Elimu Podcast; Baraza la Kiswahili; Prof. Kandagor Mosol-CHAKITA
Harakati za kuhakikisha kuwa Kenya inakuwa Baraza la Kiswahili zimeshika kasi. Wizara ya Michezo na Utamaduni imeandaa warsha (tarehe 11 na 12 Novemba, 2021) jijini Nairobi na kuwashirikisha waandishi, wahadhiri na wawakilishi wa vyama vya Kiswahili kikiwamo CHAKITA, ili kujadili suala hili. Sikiliza podcast hii ambapo Geoffrey Mung'ou anamhoji Profesa Kandagor Mosol, Mwenyekiti wa CHAKITA vilevile mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Moi.
Oct 17 2021
Elimu Podcast: Mafadhaiko miongoni mwa vijana
Mafadhaiko miongoni mwa vijana yameendelea kuwazonga na hata baadhi kukata tamaa maishani. Mwalimu Frank Otieno amezungumza kwa kina na washauri wa vijana: Evelyne Ogendo, Faith Mutendwa na Kelvin Ogada na kuangazia mbinu za kuwakwamua vijana kutokana na msongo wa mawazo nyumbani na hata shuleni.
Oct 3 2021
Elimu Podcast: TPD-Sh.6,000 kila mwaka; walimu waisuta TSC
Tume ya Huduma kwa Walimu, TSC imetoa mwelekeo wa lazima kwa walimu wote kujiendeleza kitaaluma kupitia mpango uitwao Teacher Professional Development (TPD) utakaomgharimu kila mwalimu ada ya Sh.6,000/- kila mwaka. Mwalimu Frank Otieno anazungumza na Mwalimu Benitez Osukuku kuhusu suala hili.
Sep 26 2021
Elimu Podcast: Wanafunzi Wenye Mahitaji Spesheli
Kenya inapochangamkia Mtalaa wa Umilisi (CBC), mwanafunzi mwenye mahitaji spesheli anashughulikiwaje?Mwalimu Frank Otieno amezumgumza na Daktari Festo Ndonye, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Moi, Idara ya Elimu Spesheli na Eva Nabutuni, mwandishi wa kitabu cha kufunza walimu na wazazi kuhusu elimu ya wenye mahitaji spesheli.
Sep 12 2021
Elimu Podcast: CBC Yawatatiza Wazazi na Walimu; Washikadau Wazungumza
Suala la Mtalaa wa Umilisi, CBC limezua mihemko nchini miongoni mwa wazazi, walezi, walimu na wanafunzi. Kwenye mazungumzo ya Elimu Podcast na Mwalimu Frank Otieno, tunakuletea kauli za Daktari Emmanuel Manyasa - Mtafiti wa Elimu, Daktari Janet Mangera wa FAWE-K na Serah Kimani - Mwalimu Mkuu Shule ya Demacrest. Haya yanajiri wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uwezo wa Kusoma na Kuandika, International Literacy Day. Makinika...
Sep 7 2021
Elimu Podcast: CBC Yawapa Taabu Wazazi, Walimu na Wanafunzi
Malalamishi kuhusu Mtalaa wa Umilisi, CBC yanazidi kuongezeka. Wazazi wanalalamikia gharama ya juu ya vifaa vya masomo vilevile kulalamikia suala la kutumia muda mwingi kuwasaidia wanao kufanya mazoezi waliyopewa shuleni. Baadhi yao wanapendekeza kusitishwa kwa mtalaa huo na kurejelewa kwa ule wa 8.4.4. Walimu nao wanalalama kwamba hawakupewa mafunzo yafaayo kuhusu CBC mbali na kuhitajika kufanya kazi za ziada. Wanafunzi pia wanalazimika kubeba vitabu vingi mno na kuhangaika kutafuta vifaa vinavyohitajika shuleni. Shadrack Miti amezungumza na pande zote zinazohusika. Sikiliza podcast hii kwa kina chake.
Jul 31 2021
ELIMU PODCAST; Mzigo wa karo na vitabu; wazazi wanalia
Wazazi nchini Kenya wamepaza sauti kulalamikia hatua ya Wizara ya Elimu kuwapa muda mfupi mno kujitayarisha ili kuwarejesha wanafunzi shuleni kwa muhula wa kwanza ulioanza tarehe 26, Julai, 2021. Wanafunzi takribani 15,000 wamerejea shuleni baada ya likizo ya wiki moja tu suala ambalo limewafanya wazazi kutatizika kutafuta karo na fedha za kununulia vifaa vingine kama vile vitabu. Baadhi ya wazazi walio na watoto zaidi ya mmoja, wamewarai walimu kutowarejesha wanao nyumbani kwa kutokamilisha karo wakiomba kupewa muda zaidi kujiandaa. Wengine nao wanalalamikia hatua ya baadhi ya walimu wakuu kuongeza karo kinyume na mwongozo wa Wizara ya Elimu. Aidha, wameshangaa kupokezwa orodha ndefu ya vitabu vya kusoma kuvinunua ilihali Wizara ya Elimu ilisema imevisambaza katika taasisi za elimu. Mwanahabari wetu Martin Ndiema wa Trans Nzoia amefanya mahojiano nao.
Jun 13 2021
Education Podcast: Celebrating the legacy of the late Prince Philip the Duke of Edinburgh
In celebrating the legacy of the late Prince Philip the Duke of Edinburgh, his son, Prince Edward gave an exclusive interview to Standard Group's Frank Otieno on the late Prince Philip's international award on youth and their bid to rediscover their potentials.
Jun 13 2021
ELIMU PODCAST: Usalama wa mtoto wa kike - kwenda na kutoka shuleni
Visa vya wanafunzi kudhulumiwa wanapokwenda au kutoka shuleni vinazidi kuongezeka. Baadhi wanatekwa nyara, kubakwa au kuuliwa. Je, unamwamini anayemsafirisha mtoto wako? Jamii na washikadau wote wamewajibika vya kutosha ili kukabili visa hivi? Kipi kifanywe ili kuwahakikishia watoto wa kike usalama wanapokwenda au kutoka shuleni? Mwanahabari wetu, Frank Otieno amezungumza na Teresia Otieno wa Forum for African Women Educationalists, FAWE na Dr. Susan Chang'orok Chemtai ambaye ni Mwanasosholojia kuhusu masuala haya.